Taarifa Kutoka Simba Kuhusu Hali Ya John Bocco..


Daktari mkuu wa klabu ya Simba Dr Yassin Gembe amelezea juu ya hali ya mshambuliaji wa klabu hiyo, John Bocco aliepata majeraha katika mchezo wa jana dhidi ya Mwadui fc.

 'Bocco anaendelea vizuri tofauti na hali ilivyokuwa hapo jana,  leo asubuhi tulikwenda tena hospitalini kupata matibabu ya mwanzo. Hali yake inaendelea vizuri na tutakapofika Dar es Salaam tutafanya uchunguzi' alisema Dkt.  Yassin Gembe. 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.