Posti Za Okwi Na Niyonzima Baada Ya Tarifa Za Msiba Wa Mtoto Wa Canavaro.

Tokeo la picha la okwi na nyonzima

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za  msiba alioupata beki wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub Canavaro  kwa kuondokewa na mtoto wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Okwi ameandika ujumbe unaothibisha kuumizwa kwake na msiba huo.

 Canavaro akiwa visiwa vya Ushelisheli amepata msiba wa mwanae Anwar Nadir Ally aliefariki mapema leo asubuhi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu ya matatizo ya damu.


Wakati huohuo kiungo wa klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi na raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.


Uongozi wa Sokakiganjani unatuma salaam za Rambirambi kwa Canavaro na kumuombea kwa Mungu ampe wepesi hasa katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.