Kauli Ya Kocha Yanga Mara Baada Ya Ushindi Mnono Dhidi Ya Majimaji leo


Mara baada ya mchezo kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa aliwashukuru wachezaji kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kupata ushindi ambao umeongeza nguvu ya kupata mafanikio zaidi kwenye michezo ijayo


Tumecheza vizuri,hongera kwa vijana wetu kwa namna walivyocheza na kutuhakikishia pointi tatu muhimu, limekuwa jambo jema sisi kushinda mchezo huu kwa sababu hii ni chachu kuelekea michezo ijayo, tunahitaji kuendelea kushinda ili kutenegeneza mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wetu.

Yanga Sc inataraji kuondoka nchini siku ya jumapili kuelekea Victoria huko Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji St Louis iliyopangwa kuchezwa tarahe 21/2/2018.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.