Alichosema Meneja Wa Yanga Kuhusu Mkataba Wa Donald Ngoma


Baada ya taarifa zisizokuwa rasim ambazo zimekuwa zikienea zikieleza kuwa klabu ya Yanga imeamuwa kuachana na mshambuliaji wake Donald Ngoma tayari uongozi wa klabu ya Yanga umetoa tamko juu ya taarifa hizo.

Kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo amesema bado Ngoma ana mkataba na klabu hiyo na ataendelea kusalia kunako klabu hiyo kwa misimu miwili.  
Ngoma amekuwa nje ya Uwanja kwa muda sasa kutokana na majeraha aliyonayo ya goti aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda FC.
Wiki moja iliyopita mmoja wa viongozi wa Yanga Charles  Boniphace Mkwasa alisema kuwa mchezo mchafu uliopo baina ya mchezaji na klabu hiyo huku akieleza sababu za ngoma kukosekana uwanjani zitawekwa wazi hivi karibuni.
Lakini kutokana na taarifa kutoka kwa Meneja wa Yanga Hafidh Salehe amesema kuwa anaamini kuwa Ngoma atarejea hivy karibuni. 
"Ngoma  anaendelea vizuri na naamini kuanzia wiki hii atarejea mazoezini  kabla ya kocha kumpatia nafasi katika kikoki." Alisema Hafidh.
Aidha  Meneja huyo ameongeza kwa kusema kuwa taarifa zilizokuwa zikienezwa hazina ukweli na kusema kuwa Yanga hawajavunja mkataba na Ngoma bali alikuwa na majeraha makubwa na hii ni kwa mujibu wa uchaguzi wa kitabibu uliofanyika . 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.