Dakika 90 Za Mchezo Kati Ya Yanga Na Majimaji FC Leo..


Yanga sc imefanikiwa kuvuna ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji ya Songea kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Papy Kabamba Tshishimbi ndiyo alikuwa wa kwanza kuifungia Yanga bao kufuatia mlinzi wa Majimaji kuunawa mpira uliokuwa umepigwa na Obrey Chirwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru adhabu ya penalti.

Kuingia kwa bao hilo kuliongeza harakati za mashabulizi kwa Yanga, na dakika kumi baada ya bao la kwanza Obrey Chirwa alifanikiwa kufunga bao la pili katika mchezo wa leo likiwa bao lake la 11 msimu huu kufuatia krosi ya Gadiel Michael.

Emmanuel Martin alihitimisha dakika 45 za kwanza kwa kufunga bao la tatu baada ya kufumua shuti kali akiwa umbali wa mita 30,hivyo hadi timu zote zinakwenda mapumziko Yanga ailikuwa mbele kwa bao 3-0.

Majimaji walikianza vyema kipindi cha pili na kufanikiwa kupata mkwaju wa Penalti kufuatia makosa ya walinzi wa Yanga na wageni hao kufanikiwa kupachika wavuni penati hiyo.Furaha ya timu hiyo kutoka Songea ilikoma kwenye dakika ya 54 baada ya Papy Kabamba kufunga bao la nne kwa Yanga lililohitimisha dakika 90 za mchezo huo

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.