Manyara waanza kugawa vitambulisho kwa Machinga



Mkoa wa Manyara umezindua utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo (machinga). zoezi hilo limezinduliwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Tumaini Magessa.
Magessa alisema wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye mfumo wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) hawapaswi kupatiwa vitambulisho hivyo.
“Serikali ipo pamoja nanyi wafanyabiashara wadogo, ndiyo sababu Rais John Magufuli akawatambua na kuagiza vitambulisho vyenu vitengenezwe,” alisema Magessa.
Utakumbuka December 10, 2018 Rais Magufuli alitoa vitambulisho 670, 000 na kila Mkuu wa Mkoa alikabidhiwa vitambulisho 25, 000. Kila kitambulisho kitapatikana kwa Tsh. 20, 000 kwa ajili wajasiriamali wenye mitaji usiozidi Tsh. Milioni 4.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.