Simba V Mtibwa CCM Kirumba leo


Mabingwa wa Azam Sports Federation Cup Mtibwa Sugar Sc leo wanatarajia kushuka katika dimba la CCM Kirumba leo kucheza dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao Ya Jamii.

Mtanange utakaowakutanisha mabingwa wa Azam Sports Federation Cup “kombe la shirikisho” Mtibwa Sugar na bingwa wa ligi kuu bara Simba Sc unatarajia kuwa mkali na wakipekee kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili.

Mchezo huo ambao utachezwa jijini Mwanza ni mchezo maalumu kwa ajili ya kufungua pazia la ligi kuu bara , pia mchezo huo hutumika kurudisha katika jamii hivyo asilimia ya mapato yanayopatikana katika mchezo huo hupelekwa kwa watu wenye mahitaji maalumu kwasababu lengo la mchezo huo ni kurudisha kilichopatikana kwa jamii.

Mtanange huo wa kukata na shoka unatarajia kuanza saa 10:00 jioni katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza na mgeni rasmi katika mchezo huo atakuwa ni mkuu wa mkoa Mwanza John Mongella.

Mtibwa Sugar walifanya mazoezi yao ya mwisho jana asubuhi kuelekea mchezo huo wa Ngao ya Jamii, Jumla ya wachezaji 20 wamesafiri kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji hao ni Kelvin Sabato, Juma Liuzio, Salum Chanongo, Salum Kihimbwa, Ismail Mhesa, Ally Makarani, Ayoub Semtawa, Saleh Khamis, Awadh Juma, Issa Kajia, Henry Joseph, Shaaban Mussa Nditi, Hassan Isihaka, Cassian Ponera, Dickson Job, Issa Rashid, Kibwana Ally Shomary, Rodgers Gabriel, Shaaban Kado na Benedict Tinocco

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.