MKASA WA MTIBWA SUGAR NA SIMBA KWENYE NGAO YA JAMII


Mwaka 2001, Simba SC walikuwa mabingwa wa Tanzania Bara lakini hawakupata zawadi yao baada ya mdhamini mkuu wa Ligi, (kampuni ya bia TBL kupitia bia ya Safari Lager), kujitoa katikati ya msimu.

FAT iliahidi kuwapa Simba zawadi yao pindi mdhamini mpya atakapopatikana. Mwaka 2002 Vodacom wakaja kama wadhamini wapya lakini Simba hawakupewa zawadi yao.

Kitendo cha kutopewa zawadi yao kiliwakaa rohoni Simba hadi 2009 walipogomea kucheza mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga, hadi wapewe zawadi yao ya ubingwa wa 2001.

TFF ikaachana na Simba na kuwapa nafasi hiyo Mtibwa Sugar kucheza na Yanga. Wakati huo ngao ya jamii ilizikutanisha timu zilizomaliza Ligi katika nafasi ya kwanza na ya pili.

Kitendo cha Simba, iliyomaliza katika nafasi ya pili, kugoma kikawapa nafasi Mtibwa waliomaliza katika nafasi ya tatu, kuwania ngao ya jamii.

Mtibwa hawakufanya ajizi, wakaichapa Yanga 1-0 kwa bao la Pius Kisambale na kuandika historia.

2018, Mtibwa na Simba ambao walibadilishana nafasi 2009, wanakutana...nani atafanya nini?

WASHINDI WA NGAO YA JAMII

2001 - Yanga 2-1 Simba
2009 - Mtibwa Sugar 1-0 Yanga
2010 - Yanga 0-0 Simba (Penati 3-1)
2011 - Simba 2-0 Yanga
2012 - Simba 3-2 Azam FC
2013 - Yanga 1-0 Azam FC
2014 - Yanga 3-0 Azam FC
2015 - Azam FC 0-0 Yanga (Penati 7-8)
2016 - Yanga 2-2 Azam FC (Penati 4-1)
2017 - Yanga 0-0 Simba (Penati 4-5)

By Zaka Zakazi Azam Sports

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.