Sababu ya Castal union kuvaa jezi ikiwa haina nembo ya mdhamini

Mgogoro wa kibiashara kati ya METL Group na MOFAYA wadhamini wa klabu ya Coastal Union waifanya klabu hiyo kuanza msimu na jezi zao bila kuwa na nembo ya mdhamini yoyote. Klabu hiyo ilikuwa na Jezi za aina mbili zenye nembo ya wadhamini wawili tofauti kifuani ambazo zote hawajazitumia.

METL Group ilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Coastal Union kama wadhamini wakuu ambao walikuwa kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba huo METL Group walikubali kuvunja mkataba huo ila baada ya kusikia Klabu ya Coastal Union imeingia mkataba tena na MOFAYA wakati wana mkataba na METL GROUP. Kampuni ya METL Group lilistisha mpango wa kuvunja mkataba.

Kuna hatari klabu ya Coastal Union kuingia hasara ya kuvunja mkataba wa mdhamini mmoja au kucheza ligi msimu mzima bila kuwa na mdhamini mkuu. Pia Viongozi wa klabu hiyo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na makampuni mengine mawili kuingia mkataba na klabu hiyo ila kama wadhamini wenza.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.