Lechantre aishuhudia Simba ikiidungua pressons goli akiwa jukwaani.


-Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Pierre Lechantre jana alikuwepo uwanjani kuiangalia timu yake ya zamani (Simba) ikicheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya TZ Prisons na Simba ikashinda kwa goli moja kwa bila (1-0). Alipoulizwa kuhusu Performance ya Simba dhidi Tz Prisons, Lechantre alijibu kifupi 'No Comment'

-Kwa sasa Kocha huyo yupo nchini ametumwa na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) kuangalia mashindano ya kufuzu kwa Afcon U 17, 2019 kwa kanda ya Afrika mashariki na kati (CECAFA) yanayofanyika Tanzania na sasa yamefikia hatua ya nusu Fainali. Michezo ya nusu fainali itachezwa kesho Ethiopia dhidi ya Rwanda na Tanzania dhidi ya Uganda.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.