Kocha Yanga azitupia kombora Simba na Azam


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kikosawa licha ya kuwa wao hawakuweka kambi ya kujiandaa na ligi katika majiji makubwa na hata kwenda katika nchi za watu.

Akizungumza  na gazeti la mwanaspoti Zahera amesema kuwa kambi yao ilikua nzuri na hivyo imewajenga wachezaji na kudriki kurusha kombora kwa timu za Simba na Azam zilizoweka kambi Uturuki na Uganda

''Tulikuwa na wiki mbili za mazoezi Morogoro kwa sasa timu ilivyo naweza kusema tunaweza  kuwa katika usawa na na timu nyingine kama zile zilizoenda Uturuki na hata Uganda katika ubora''
        '' Timu sasa imeimarika nafurahi tuna kikosi imara cha kushindana na timu yoyote, wachezaji tuliowaongeza wameleta nguvu na ukiongeza na hawa waliokuwepo timu yetu ipo vizuri.

Mwinyi Zahera,
Kocha Mkuu , Yanga SC

(Source :Mwanaspoti)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.