Kessy aanza vitu vyake atwaa tuzo ya kwanza Zambia.

-Beki wa zamani wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy jana alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya ligi kuu Zambia Kati ya Nkana Red Devils dhidi ya Kabwe Warriors. Kessy ameshinda tuzo hiyo kwa kuchaguliwa na mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuisaidia Nkana Red Devels kushinda kwa magoli mawili kwa bila (2-0) na kuzawadiwa Kwacha 1,000 ambayo ni zaidi ya  200,000 za Kitanzania.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.