Yanga Yakubali Kipigo Kutoka Kwa Mwadui Yafikisha Game 9 Bila Ushindi.
Timu ya soka ya Yanga leo hii imeendelea kugawa takrima kwa timu za ligi kuu za Tanzania Bara kwani, baada ya kufungwa 1-0 na Mwadui FC.
Huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Yanga kupoteza, baada ya kufungwa bao 2-0 na Tanzania Prisons na baadae kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar huko Turiani mkoani Morogoro wiki iliyopita.
Yanga sasa imefikisha michezo tisa mfululizo bila kupata ushindi katika mashindano yote ambayo imeshiriki katika miezi ya hivi karibuni.
Yanga imekuwa kama pombe ya ngomani kila mtu anajichotea kwani imekuwa na msimu mbaya kabisa kulinganisha na misimu ya hivi karibuni.
Yanga inabakia katika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia alama 48 nyuma ya Azam FC.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.