Chelsea Waibamiza Manchester United, Watwaa Ubingwa Wa FA.

Chelsea imetawazwa mabingwa wapya wa kombe la FA baada ya kuifunga Manchester United bao moja katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Wembley.

Bao pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na Eden Hazard kwa mkwaju wa penati dakika ya 22 baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi Phil Jones.

United ilimiliki sehemu kubwa ya mchezo huo ikifanya mashambulizi mengi langoni mwa Chelsea lakini hawakufanikiwa kupata bao la kusawazisha.

Chelsea walifanya mashambulizi machache ya kushtukiza wakitumia mipira mirefu wakimtumia Hazard na Oliver Giroud walio ongoza safu ya ushambuliaji.

Arsenal ndio walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kuifunga Chelsea mabao 2-1.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.