Rais Magufuli: “Kwa mpira huu wa leo Simba hamuwezi kuchukua kombe la Afrika"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameituma klabu ya Simba kuleta kombe la Klabu Bingwa barani Afrika ili awakabidhi kwa mara nyingie baada ya kushinda taji la Ligi kuu Tanzania bara.
Magufuli amewataka wachezaji na viongozi wa Simba kujipanga vizuri ili kufanya vizuri kimataifa lengo kulileta kombe hilo hapa Tanzania na wamualike tena aje kuwakabidhi.
“Nitafurahi sana siku moja vilabu vya Tanzania na timu ya taifa ikaleta kombe hilo hapa na niwakabidhi Simba. Mmechukua taji la ligi kuu Tanzania sasa mkachukue taji la Afrika mwakani,” Rais Magufuli alisema.
Katika hatua nyingine amewaambia Simba kwa namna alivyoiangalia Simba siku ya leo haiwezi kuchukua ubingwa endapo itacheza kama ilivyocheza leo.
“Kwa mpira huu wa leo Simba hamuwezi kuchukua kombe la Afrika, mbadilike mcheze zaidi ya hapa, mie nawaambia ukweli sikuzote,” amesema.
Katika hatua nyingine Magufuli amewaacha hoi wapenzi na mashabiki waliohudhuria uwanjani akikumbushia baadhi ya matukio yaliyotokea kipindi hca nyuma ikiwemo kuvunjwa kwa viti pamoja na kupelekea kesi FIFA.
“Nafurahi msimu huu hakuna timu iliyoenda FIFA kudai haki, inaonekana namna gani uongozi huu uko vizuri,” amesema.
Kartika mchezo huo Simba imepoteza kwa mara ya kwanza baada ya kucheza michezo 28 ambapo imeshindwa kuitengeneza rekodi yao waliyoiweka msimu wa 2009-2010
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.