Yanga Kuitumia Siku Hii Kumtambulisha Mrithi Wa Ngoma

Klabu ya Yanga itatumia michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza Jumapili ya Juni 03 nchini Kenya kumtambulisha mshambuliaji wake mpya atakayechukua nafasi ya Donald Ngoma.

Yanga ilifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa Ngoma baada ya kushindwa kupona majeraha yake kwa muda mrefu.

Ngoma tayari amesajiliwa na klabu ya Azam FC ambapo leo imethibitisha rasmi juu ya usajili wake na kueleza kuwa mchezaji huyo anapelekwa Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi wa majeraha yake.

Yanga tayari ina orodha ya majina ya wachezaji wanne wa kigeni wanaotarajiwa kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria wa soka la Tanzania

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.