Azam yamkana Pluijm
Hivi karibun i baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza Pluijm kuwa mbioni kujiunga na Azam FC na kuachana na Singida United.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, pamoja na taarifa hizo kuenea, Makamu Mwenyekiti wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat', alikana klabu yake kumchukua kocha huyo wa zamani wa Yanga.
"Si kweli taarifa hizo, kama kuna jambo hilo au mazungumzo mtafahamu ila hakuna ukweli wowote juu ya kocha Pluijm," alisema Popat.
Aidha, alisema kocha wao wa sasa, Aristica Cioaba mkataba wake unamalizika mwezi Julai hivyo kama kuna jambo lolote watalizungumza na kuliweka wazi.
Akizungumzia maandalizi ya msimu ujao kwa timu yake, alisema watakiboresha kikosi chao kwenye safu ya ushambuliaji, beki wa kushoto na kiungo.
Kuelekea mwisho wa msimu huu, kocha Pluijm amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Azam na tayari ameshaaga kwenye kikosi chake cha Singida United.
Azam inawania kumaliza ligi kwenye nafasi ya pili na wanachuana na Yanga kuwania nafasi hiyo, timu hizo zitakutana kwenye mchezo wa mwisho msimu huu, jumatatu usiku.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.