Uongozi Yanga Watoa Mwongozo Kwa Wanachama Wake


Uongozi wa Klabu ya Young Aficans SC (Yanga) umeurudisha nyuma mkutano mkuu wa wanachama wake ambao ulitakiwa kufanyika Jumapili Juni 17, 2018 na badala yake sasa utafanyika Juni 10 bila ya kutoa sababu maalum za kufanya hivyo.



Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Utendaji ya wanajangwani na mchana wa jana Mei 27, 2018 na kusema ukumbi utakaotumika kwaajili ya mkutano huo, utatangazwa katika siku za baadaye.

Aidha, taarifa hiyo licha ya kutoweka dhumuni ya mkutano huo imewasisitizia wanachama wake kuwa mkutano huo utawahusu wale wote wenye kadi za uanachama mpya na zile za zamani.

"Jambo la kuzingatia ni kwamba lazima kadi hizo ziwe hai yaani zimelipiwa ada na mwanachama lazima awepo kwenye 'register' ya klabu na tawi lake", imesema taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine, Yanga inatarajia kushuka dimbani leo Mei 28, 2018 kuvaana na Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.