Ujumbe Mzito Wa Lwandamina Kwa Yanga


KOCHA wa zamani wa Yanga, George Lwandamina ameipa neno timu hiyo endapo inahitaji kusonga mbele na kujikwamua kwenye hali waliyonayo sasa.


Lwandamina ambaye aliikacha klabu hiyo mapema mwezi Aprili, alisema njia kamili ya timu hiyo kujikwamua katika matatizo yanayowakabili sasa zaidi ya kuwa na mshikamo na kujipanga upya.


Kocha huyo raia wa Zambia aliondoka Yanga kutokana na hali ngumu ya kifedha pamoja na matatizo ya kiutendaji na tangu kuondoka kwake timu hiyo imeshinda mchezo mmoja tu kati ya 10 iliyocheza.


"Umoja ni jambo muhimu wakati wa kutafuta mafanikio, mnapoungana na kuwa kitu kimoja katika kila jambo mnalifanya kwa nguvu na ushirikiano mtafanikiwa," alisema Lwandamina kwa njia ya simu kutoka kwao Zambia.


"Pia, mipango hiyo inatakiwa kufanywa kisasa na kuacha mambo ya mazoea na ujuaji kwani mafanikio yoyote ni mipango."

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.