Yanga Kuisaka Nafasi Ya Pili Leo.


Leo jioni Yanga itakuwa uwanja wa Taifa ikicheza na Ruvu Shooting kukamilisha ratiba yake ya 'viporo' kuelekea mwishoni mwa msimu.

Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo bila ya presha kubwa hasa baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na uimara wa Ruvu Shooting ambayo inashika nafasi ya nane ikiwa imejikusanyia alama 36.

Yanga leo huenda ikawatumia baadhi ya wachezaji wake waliokosa mchezo dhidi ya Mbao FC kutokana na sababu mbalimbali.

Andrew Vicenct Chikupe, Papi Tshishimbi na Ibrahim Ajib ni miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuwemo kwenye kikosi cha Yanga leo.

Chikupe amemaliza adhabu ya kadi tatu za njano wakati Tshishimbi amerejea kutoka kwenye majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani wiki tatu.

Ajib amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa wiki mbili akimuuguza mkewe aliyejifungua hivi karibuni

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.