Juma Luizio Ajipanga Kuondoka Simba.
WAKATI viongozi wa Simba wakisubiri ripoti ya kocha wao Pierre Lechantre kujua ni wachezaji gani atawapiga panga na anahitaji sura gani mpya, straika wa timu hiyo, Juma Luizio ameanza hesabu zake mapema.
Luizio aliliambia Mwanaspoti ana furaha kuona Simba imetwaa ubingwa na yeye amevaa medali, lakini anahitaji kukiokoa kipaji chake, huku akizipigia hesabu timu anazoziona zinaweza kumfaa kuwa ni Singida United, Lipuli, Mtibwa Sugar na Azam FC.
"Sitaki kwenda timu ili mradi tu, nahitaji kucheza na kupata ushindani wa kufanya nijitume, hizo timu nilizozitaja zinaonekana zina malengo katika Ligi Kuu.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.