Tetesi Zote za Usajili Ulaya Leo Jumapili May 20.2018


Imethibitishwa kuwa kiungo Emre Can ataondoka kutoka Liverpool kwenda kwa Juventus. (Sunday Express)

Everton imejiunga kwenye mbio za kumuwania mshambuliaj wa timu ya taifa Ivory Coast na Crystal Palace Wlfried Zaha, 25 kwa kitita cha pauni milioni 60(Sun on Sunday)

Maisha ya kiungo Marouane Fellaini ndani ya Manchester United yanaonekana kufika mwisho baada ya mchezaji huyo kuhama katika nyumba yake Cheshire, vilabu vya monaco, Marseille vinavutiwa kumsajili mchazaji huyo.(Sunday People)

Tottenham inataka kumsajili kiungo wa kati mwenye asili ya Colombia,Barrios, 24, kutoka Boca Juniors ya Argentina.(Sun on Sunday)

Juventus wana mpango wa kurudi kuhitaji sahihi ya nyota wa Arsenal Hector Bellerin kama klabu yake itapunguza dau la pauni milioni 50 inayotakiwa kumuachia mchezaji huyo. (Sunday Express)

Besiktas wako tayari kumsajili mshambuliaji Alfredo Morelos 21 wa Rangers kwa mkopo.(Daily Record)

Meneja wa zamani wa Hammers David Moyes alishtuka baada ya mkataba wake kutosajiliwa upya baada ya kuahidiwa mkataba mwingine wiki nne zilizopita.(Sun on Sunday)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amekuwa na majadiliano chanya na klabu kuhusu mustakabali wake, huku chelsea ikiwa imeshindwa kumpeleka Stamford Bridge raia huyo wa Argentina.(Sunday Telegraph)

Zenit St Petersburg wanamfuatilia meneja Rafael Benitez ndani ya New Castle United. (Newcastle Chronicle)

Crystal Palace wanavutiwa na kumsajili beki wa kulia Ryan Fredericks mwenye miaka 25 ambaye mkataba wake unakaribia kufikia mwishoni Carven Cottage.(Sunday Express)

Everton ina matumaini ya kumtangaza meneja wao mpya Marco Silva, meneja wa zamani wa Watford mwanzoni mwa juma lijalo. (Mail on Sunday)

Liverpool wamefuta mpango wa kucheza mechi za majaribio kabla ya msimu ujao dhidi ya klabu ya borussia Monchengladbach kwa kuwa klabu hiyo inamfuatilia mshambuliaji wake Rhian Brewster, 18. (Liverpool Echo)

Zaidi ya mashabiki 2,000 wa Real Madrid wamerudisha tiketi zao za mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Jumamosi ijayo dhidi ya Liverpool(Independet)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.