Ligi Kuu Tanzania Bara Kufikia Tamati Leo Je Simba Wataweka Heshima? Na Yanga Je Wataikamata Nafasi Ya Pili?.






Patashika Nguo kuchanika pale ambapo kikomo cha ligi kuu kwa msimu wa mwaka 2017/2018 kukamilika.




Katika kuelekea ukingoni leo kuna vita kuu mbili ambapo ya kwanza ni ile ya kumtafuta atakayeshika nafasi ya pili na ile ya atakayesalia kwenye ligi kwa msimu ujao.




Katika kuhakikisha nafasi ya pili Yanga watapambana na Azam kwenye mtanange wa mwisho huku timu zote zikiikodolea macho nafasi hiyo.




Katika hatua nyingine Majimaji ya Songea itakuwa dimbani kuwakaribisha Simba huku ikiwa na matumaini ya kushinda na kuwaombea njaa Ndanda fc ambao watakuwa dimbani kuwakaribisha Stand United.




Ikumbukwe kuwa Njombe Mji ndio klabu pekee ambayo tayari imeshuka daraja.




RATIBA KAMILI HII HAPA.Yanga SC vs Azam FC - Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam (Saa 2:00 Usiku)

Majimaji FC vs Simba SC - Uwanja wa Majimaji, Songea (Saa 10:00 Jioni)

Ndanda FC vs Stand United - Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara (Saa 10:00 Jioni)

Lipuli vs Kagera Sugar - Uwanja wa Samora, Iringa (Saa 10:00 Jioni)

Tanzania Prisons vs Singida United - Uwanja wa Sokoine, Mbeya (Saa 10:00 Jioni)

Njombe Mji vs Mwadui FC - Uwanja wa Sabasaba, Njombe (Saa 10:00 Jioni)

Mbao FC vs Ruvu Shooting FC - Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza (Saa 10:00 Jioni)

Mtibwa Sugar vs Mbeya City - Uwanja wa Jamhuri, Morogoro (Saa 10:00 Jioni)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.