NYIKA: HATUKUPANGWA KUNDI JEPESI KAMA MNAVYODHANI
Uongozi wa Yanga umesema haujapangwa katika kundi jepesi la kombe la Shirikisho Afrika kama watu wengi wanavyodhani na wanahitaji kujiandaa vizuri ili kufika hatua ya robo fainali.
Baada ya droo iliyofanyika jana jijini Cairo, Yanga imepangwa kundi D pamoja na timu za USM Algier, Gor Mahia na Rayon Sports.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika amesema kila timu iliyoingia hatua hiyo ni bora ndio maana imefika hapo kwahiyo watu wasidhani kuwa wapo kwenye kundi jepesi.
"Kundi letu sio jepesi kama wengi wanavyodhani, Gor au Rayon sio timu ndogo hata kidogo tupasawa kujipanga vilivyo," alisema Nyika.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa faida waliyopata kipindi hiki ni kucheza karibu hivyo wachezaji hawatakuwa na uchovu wa safari.
Katika kundi hilo timu za Yanga, Gor na Rayon zinatoka ukanda wa Afrika Mashariki wakati Alger ndio inatoka Afrika Kaskazini.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.