Azam Fc wakubali matokeo wahamishia nguvu kwenye ligi kuu



Baada ya kuondolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya ASFC timu ya Azam sasa imeelekeza nguvu yake kwenye ligi kuu ambapo wanajiandaa kwa mchezo dhidi ya Timu ya Mbeya City.

Afisa Habari wa Klabu ya Azam amesema kuwa wamekubali matokeo na kuwa watajipanga upya kwa ajili ya michuano hiyo msimu ujao.

"Tumekubali matokeo ya mchezo dhidi ya Mtibwa kombe la FA tumeondolewa kwenye mashindano na tumekubali matokeo asiyekubali kushindwa si mshindani mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa mtibwa ni timu nzuri sasa hivi tunaangalia mbele zaidi katika ligi kuu Tanzania bara ambapo mchezo unaofuata tunacheza na Mbeya City tunajiandaa na tutaanza mazoezi Jumatatu", amesema Maganga.

Ugenini

Katika mchezo huo ambao utafanyika Aprili 08 2018, Azam Fc ambao wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 44 alama mbili nyuma ya Simba na Yanga watakuwa ugenini

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.