Mabadiliko: Yanga Kama Ulaya, Sasa kuwaweka Mashabiki Pamoja Kwa Nyimbo


Uongozi wa Yanga umedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ikiwa sasa kwenye mipango ya kuisogeza klabu karibu zaidi na mashabiki wake.

Ndio! Tumezoea kule katika ligi kubwa barani Ulaya hasa Uingereza ambako wengi tumekuwa tukifuatilia kwa ukaribu, timu kama Manchester United, Liverpool, Arsenal etc zina nyimbo maalumu ambazo ni kama nyimbo za Taifa za klabu.

Ukienda pale Anfield, kwenye uwanja wa Liverpool mashabiki wa klabu hiyo kongwe kabisa nchini Uingereza huanikiza na wimbo wao maarufu sana 'You will Never Walk Alone'.

Pale Old Trafford utakaribishwa na wimbo wa 'Go Go Manchester United' au pale Emirates dimba la Arsenal utakaribishwa na 'Arsenal we're on your side'

Hali huwa ni hivyo hivyo ukienda Nou Camp, uwanja wa FC Barcelona. Kabla ya kuwavaa wababe hao wa soka la Hispania, timu yao huwa inaingia uwanjani na wimbo wao maalum 'El Cant del Barca'

Yanga nayo imefuata mkumbo huo na sasa tayari iko kwenye mchakato wa kuandaa wimbo maalum ambao utaitambulisha klabu mahali popote.

Kwa yeyote anayefahamu kuandika vyema mashairi uongozi wa Yanga umemtaka kuwasiliana nao kupitia barua pepe info@yangasc.co.tz 

Miaka ya 90 wakati huo Yanga ikifadhiliwa na mfanyabiashara marehemu Abasi Gulamali, iliwahi kutungiwa wimbo na gwiji wa muziki wa dansi kutoka Congo DRC, marehemu Pepe Kalle ulioitwa 'Young Africans'.

Wimbo huu ulitungwa na Pepe Kalle miaka hiyo alipofanya ziara nchini Tanzania wakati ambao Yanga ilikuwa imetoka kutwaa taji la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati.

Mpaka leo wimbo ndio umekuwa ukitumika kuitambulisha Yanga katika shughuli mbalimbali licha ya kwamba umepitwa na wakati


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.