Wachezaji 7 Watakaoachwa Simba Msimu Huu

Wakati tukielekea ukingoni mwa ligi kuu Tanzania bara baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha Simba huenda wakaachwa kutokana na kutokuwa na nafasi kwenye kikosi cha Mfaransa Pierre Lechantre.

Miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakawa wa kwanza kuachwa ni Mohamed Ibrahim 'MO' hii ni kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na Kocha Lechantre.

Kiungo huyo ambaye kwa miezi kadhaa sasa amekosekana kwenye kikosi cha Simba huenda akajiunga na wapinzani wa Simba, "Yanga".. Na endapo mambo hayatakuwa  sawa basi itakuwa ni nafasi yake sasa kuamua ni timu ipi atakuwa tayari kujiunga nayo.


Juma Luizio na Laudit Mavugo nao pia wanatajwa kuondoka klabuni humo ifikapo mwishoni mwa msimu hu. 

Mchezaji mwingine ni Mwinyi Kazimoto ambaye anatarajiwa kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu.

Aidha kwa mujibu wa fununu ni kuwa mchezaji kipenzi cha mashabiki wa Simba, Mohamed Hussein "Tshabalala" nae huenda akaachwa msimu huu utakapokuwa umemalizika.

Wengine ni Jamali Mwambeleko na Paul Bukaba ambao wamejiunga na klabu hii  mwanzoni mwa msimu huu na kutokuwa na msimu mzuri.
Simba kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kwa alama 59 ikiwa ni pointi 11 mbele ya mahasinu wao Yanga wenye pointi 48.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.