+PICHA Yanga Walivyofanya Mazoezi Jana Kuelekea Mchezo Wa Kesho.



Kikosi cha Yanga jana jioni kilifanya mazoezi kwenye Old Stadium mji wa Awassa kujiandaa na mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi wenyeji wao Wolaitta Dicha.

Yanga iliwasili katika mji huo juzi. Mchezo dhidi ya Dicha utapigwa dimbani hapo kesho Jumatano, April 18 2018.

Huku ikiwa tayari inaongoza kwa mabao 2-0 ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza uliopigwa April 07 kwenye uwanja wa Taifa, Yanga inahitaji matokeo ya sare au ushindi ili kutinga hatua ya makundi.

Hata ikifungwa kwa bao 1-0 Yanga bado itatinga hatua ya makundi. Ikipata bao la ugenini itaiongezea mlima Dicha ambapo italazimika kushinda kwa mabao 4-1.

+PICHA WACHEZAJI YANGA WAKIWA MAZOEZINI






No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.