MECHI YA LIPULI DHIDI YA SIMBA YASOGEZWA MBELE


Mchezo wa ligi kuu baina ya Lipuli FC dhidi ya Simba uliokuwa uchezwe Aprili 20 katika uwanja wa Samora mkoani Iringa umesogezwa mbele siku moja sasa utapigwa Aprili 21.

Uamuzi wa kusogeza mechi hiyo umetokana na uwanja wa Samora unaomilikiwa na Chama cha Mapinduzi kuwa na shughuli nyingine siku hiyo

Taarifa iliyotolewa na Mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi, Boniface Wambura jioni hii imesema mechi hiyo ilipangwa kufanyika siku ya Ijumaa lakini sasa itapigwa Jumamosi.

Hii sio mara ya kwanza kwa mechi kusogezwa mbele au kuahirishwa kwa sababu ya viwanja kuwa na matumizi mengine kwakua timu nyingi hazina viwanja.

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa kileleni mwa msimamo na pointi 58 huku ikiizidi Yanga ambao wapo nafasi ya pili kwa alama 11.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.