NGOMA NJE, NIYONZIMA NJE, PAPY TSHISHIBI 50/50

Na Joseph michael
-Kuelekea mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga kesho jumapili ya April 29 katika uwanja wa Taifa Dar. Hali ya vikosi vyote viko salama isipokuwa Donald Ngoma kwa upande wa Yanga na Haruna Niyonzima kwa upande wa Simba watakosekana.

-Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga wamerejea jana jijini Dar wakitokea Mkoani Morogoro walipoweka kambi ya Siku nne kujiandaa na mchezo huo.

-Akiongea na waandishi wa habari hapo jana mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema mshambuliaji wao wa kimataifa wa Zimbambwe, Donald Ngomba ni mchezaji pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo wa kesho kutokana na kuwa na majeruhi.

-Pia Ten amewaomba mashabiki wa klabu hiyo wamvumilie Ngoma kwani bado anaendelea kuuguza majeraha yake. Ten amewakumbusha mashabiki wa klabu hiyo ni kawaida kwa mchezaji kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu hajànza Ngoma kwani hata ulaya kuna wachezaji wanakaa nje ya uwanja hata kwa msimu mzima anewaomba mashabiki wawe na uvumilivu na Ngoma.

-Ikiwa kwa upande wa Yanga wakimukosa Ngoma upande wa Simba watamkosa Fundi wao wa mpira Haruna Niyonzima ambaye yuko kwao Rwanda kwenye msiba wa dada yake. na hatakuwepo kwenye mchezo wa watani wa jadi hapo kesho.

-Pia Kiungo wa klabu ya Yanga Papy Kabamba  Tshishimbi yupo hatihati kucheza mchezo wa kesho baada ya jana asubuhi kushindwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake, Papy ambaye aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa Caf Confederation Cup dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia jumanne ya wiki hii alirejea na kujiunga na kambi mkoani Morogoro na kufanya mazoezi na wenzake ila jana alhamisi hakuweza kufanya mazoezi.

-Daktari wa Klabu ya Yanga, Edward Bavu amethibitisha hilo akadai bado muda upo na watafanya kila namna Kiungo huyo acheze mchezo huo. Papy hakufanya mazoezi leo(jana) asubuhi na wenzake ila kesho (leo) jioni watajua kama atacheza mchezo wa jumapili au laah.

-Vilabu vya Simba na Yanga zitashuka kwenye uwanja wa Taifa Dar kesho majira ya saa 10:00 jioni huku klabu ya Simba wakiwa wanaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kwa Pointi 59 na wakifuatiwa na Yanga waliopo nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 48 ingawa Simba wamecheza michezo 2 zaidi ya Yanga

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.