MTAFUNO WAENDELEA KWA SIMBA QUEENS

Na Joseph michael
FT Simba Queens 0-2 Panama Fc

Simba Queens imeendelea kufungwa katika muendelezo wa ligi kuu ya wanawake Serengeti Lite Women's Premier League Super 8 kwa kufungwa magoli mawili kwa bili (2-0) na Panama Fc ya Iringa katika Dimba la Karume jijini Dar na hii ni mechi ya 5 kufungwa.

-Kwa matokeo hayo Simba wameshuka kwa nafasi moja kwenye msimamo wa ligi kuu ya Wanawake kutoka nafasi ya 6 mpaka 7 huku Panama Fc wao wakipanda kutoka 7 kwenda 6.

Matokeo Mengine

FT Kigoma Sisterz 1-2 JKT Queens
FT Mlandizi Queens 3-1 Alliance Girls

Ratiba ya kesho
Boabab Queens va Evergreen Queens

Msimamo
  Timu                             P    GD   Pts
1-JKT Queens               6     29    18
2-Mlandizi Queens       6     11    12
3-Kigoma Sisterz          6     04    12
4-Alliance Girls             6    -02    10
5-BaoBab Queens        5    -08    05
6-Panama Fc                6    -09    05
7-Simba Queens          6    -10    03
8-Evergreen Queens   5    -15    01

NB-Kwa Ligi hii hamna timu ambayo inashuka Daraja hii ni Super 8 kulikuwa na timu 12 ambazo zilishiriki ligi ya wanawake timu zilipangwa makundi mawili A na B kila kundi likiwa na timu 6

-Timu zilizoshika nafasi za nne za juu ndio zilifuzu nane bora (super 8) na zile timu 2 ambazo zilizoshika nafasi ya mwisho kwa kila kundi ndio zilizoshuka daraja.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.