Yanga Wagundua Janja Ya Township Rollers Mchezo Wa Marudiano..
Katika kuelekea mchezo wa mrudiano baina ya klabu ya Yanga na Township Rollers unaotarajiwa kupigwa mnamo tarehe 17 mwezi huu katika mji wa Gaborone nchini Botswana.
Straika wa Yanga, Emmanuel Martin, amegundua janja ya wapinzani wao hao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kwamba huenda wana wachezaji wazuri ambao hawajawatumia, jambo linalowafanya waongeze umakini.
Yanga ambayo katika mchezo wa awali ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilipoteza kwa kufungwa na magoli 2-1 kitu kinachopelekea kuwa katika wakati mgumu wa kuhakikisha wanafanya juu chini kuhakikisha wanapindua matokeo hayo na kusonga mbele katika michuanihiyo.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.