Tottenham na Manchester City Zakubali Vipigo, Haya Hapa Matokeo ,timu zilizofuzu Robo Fainali Na Ratiba Ya UEFA michezo ijayo..

Klabu za Tottenham na Manchester City zimekubali vipigo katika michezo yao ya pili ya raundi ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya.

Matokeo hayo yameigharimu zaidi timu ya Tottenham ambayo katika mchezo wa awali ilitoa sare ya goli 2-2 ugenini na hivyo kutupwa nje ya michuabo hiyo kwa agrigate ya goli 4-3 baada ya kupoteza kwa mabao 2-1.

Kwa upande wa Mancheser City licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-2 kutokana na ushindi wa awali ugenini dhid ya FC Basel.

Tayari mpaka sasa timu  nne zimekwisha kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Timu hizo ni:-
Juventus
Liverpool
Manchester City na Real Madrid.

Imebakia michezo minne ambayo inatarajiwa kupigwa wiki ijayo ambapo Mashetani wekundu watahuka dimbani kumenyana na Sevilla huku Chelsea wao wakiwafuata Barcelona uganini..


No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.