TETESI ZOTE ZA USAJILI ULAYA LEO IJUMAA MACHI 16.2018

Chelsea wanamfuatilia kwa karibu
kiungo wa kati wa Wales anayechezea Arsenal Aaron Ramsey, 27, ambaye
amesalia na mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake wa sasa Gunners.
Ramsey bado hajatia saini mkataba mpya. (Mirror)
Barcelona
wanaamini Andres Iniesta ataihama klabu hiyo na kujiunga na klabu moja
Uchina mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 33 utakapomalizika mwisho wa
msimu. (Sport)
Juventus
wamekutana na mawakala wa Anthony Martial, 22. Klabu hiyo ya Italia
inataka sana kumnunua mchezaji huyo Mfaransa anayechezea Manchester
United. (Premium Sport - in Italian)
Chelsea wana wasiwasi mkubwa kwamba Eden Hazard na
kipa wao Thibaut Courtois wanaweza kumfuata meneja wao Antonio Conte
katika kuihama klabu hiyo iwapo Blues hawatafanikiwa kufuzu kwa Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. Wawili hao wamekuwa wakitafutwa na Real
Madrid kwa muda. Paris St-Germain wa Ufaransa pia wanawafuatilia wawili
hao kwa karibu. (Mirror)
Real Betis wanaamini kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere
alitoa matumaini kwamba angehamia kwao ili kupata nafasi nzuri ya
kujadiliana mkataba mpya na Gunners. (Sun)
Manchester United
walifuta ziara ya wachezaji wa klabu hiyo kwenda kuhudhuria Tamasha ya
Cheltenham Festival baada ya klabu hiyo kuondolewa kutoka Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya Jumanne. (Independent)
Alipoulizwa iwapo anapanga kuwachezea Sweden katika
Kombe la Dunia baadaye mwaka huu, mshambuliaji wa Manchester United
Zlatan Ibrahimovic, 36, alijibu: "Nikitaka, nitakuwa huko". (Daily
Mail)
Mshambuliaji wa zamani wa Romania Adrian Mutu, aliyecheza
chini ya Jose Mourinho katika klabu ya Chelsea, amedai kwamba si kweli
kuwa Ibrahimovic ameumia. Amesema ukweli ni kwamba hachezeshwi katika
Manchester United kwa sababu alizozana na Mourinho. (Telekom Sport - kwa
Kiromania)
Arsenal wanapanga kumpa kiungo wa kati kutoka Misri Mohamed Elneny, 25, mkataba mpya. (Mirror)
Pasipoti
ya Danny Ward ilipotea alipokuwa anawasilisha ombi la viza ya kwenda
China. Kipa huyo wa Liverpool mwenye miaka 24 hivyo basi hataweza
kusafiri na timu ya Wales kucheza michuano ya Kombe la China. (Times)
Wamiliki wenza wa West Ham David Sullivan na David
Gold wanakusudia kuhudhuria mechi ijayo ya nyumbani ya klabu hiyo licha
ya kwanza mashabiki wa timu hiyo walizua fujo katika uwanja huo wa
London wiki iliyopita. (Sun)
Walinzi watano walijeruhiwa na
mashabiki wa Marseille waliokuwa wamesafiri Uhispania kwa mechi ya
Europa League Alhamisi dhidi ya Athletic Bilbao. (El Periodico)
Wenger: Ilikuwa muhimu kuwavutia tena mashabiki
Mashabiki
sugu kati ya 100 na 150 wa klabu ya Lyon ya Ufaransa waliwashambulia
polisi nje ya uwanja wa klabu hiyo kabla ya mechi yao ya Europa League
Alhamisi dhidi ya CSKA Moscow. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanataka
mchezaji wa zamani wa Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid Xabi
Alonso, ambaye kwa sasa amestaafu, afungwe jela miaka minane unusu kwa
kosa la kutumia ulaghai wakati wa kulipa kodi. (El Mundo - kwa
Kihispania)
Join us on
WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.