Kuhusu Figisu Za Waarabu Simba Waeleza Haya..
Akihojiwa katika kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM, Meneja wa klabu ya Simba Richard Robert amesema wameridhishwa na mapokezi waliyopewa na wenyeji wao, Al Masry nchini Misri.
Kulikuwa na hofu kwamba Al Masry huenda ingefuata utamaduni wa miaka mingi wa timu za Misri kufanya 'figisu' kwa timu zinazofika nchini humo.
Baada ya kutua jijini Cairo Simba ilitumia usafiri wa basi kwenda jiji la Port Said ambako ndiko yaliko makazi ya klabu ya Al Masry na ndiko utakakopigwa mchezo baina ya timu hizo.
Aidha, Robert amesema hali ya hewa ilivyo ndani ya jiji la Port Said ni baridi, hivyo wameanza mazoezi majira ya usiku ili kuizoea hali hiyo kwa haraka.
Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.