TAARIFA MPYA KUTOKA SIMBA JIONI HII..

SIMBA SPORTS CLUB
  DAR ES SALAAM
     5/3/2018

  *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

Makocha Hossam Hassan wa Timu ya Al-Masry na Pierre Lechantre wa Simba kesho saa tano asubuhi watazungumza na Wanahabari Kuelekea mchezo wao wa kombe la Shirikisho utakaopigwa siku ya Jumatano ya tarehe saba mwezi huu.

Mkutano huo muhimu utafanyika kwenye ukumbi wa Kivukoni four uliopo ktk Hoteli ya Nyota tano ya Serena iliyopo hapa jijini.

*Wakati huo huo* Waziri wa kilimo wa Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mh Charles Tizeba* anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanasimba na watanzania kuishangilia Simba kwenye mchezo huo utakaoanza saa kumi na mbili jioni.

Mh Tizeba ndio mgeni rasmi katika mchezo huo ambao utachezeshwa na Waamuzi toka nchini Afrika kusini.

IMETOLEWA NA
HAJI S  MANARA

MKUU WA HABARI
SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.