Pambazuka Na Habari Kubwa Kutoka Simba SC Asubuhi Hii.


==>Taari ya kwanza tuliyonayo kutoka Simba ni kuwa Mshambuliaji John Bocco, Salim Mbonde pamoja na Haruna Niyonzima wameanza kufanya mazoezi na kikosi cha Simba wakati kikosi kikiendelea na mazoezi yake kujiandaa na mchezo unaofuata kwenye ligi kuu dhidi ya Njombe Mji FC katika uwanja wa Boko jijiini Dar es Salaam.

==>Kiungowa Simba Jonas Mkude ameumia kifundo cha mguu wa kulia (Ankle) akiwa mazoezini jana jioni.

Kwa mujibu wa Daktari wa kikosi cha Simba Yassin Gembe amesema kuwa majeraha hayo aliyoyapata Mkude sio makubwa kwa mujibu wa vipimo vya awali na kuongeza kuwa leo itatoka taarifa kamili kuhusiana na hali yake kwa ujumla.

 'Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali sio majeraha makubwa sana, ila kesho ndio tutatoa taarifa kamili kuhusianana na hali yake kwa ujumla ila kwa sasa napenda kusema anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia'

==>Bodi ya Ligi jana iiitoa ratiba mpya ya michezo iliyobaki ya ligi kuu ya Vodacom ambapo mchezo kati ya Njombe Mji dhidi ya Simba utapigwa April 03.

Njombe Mji imekuwa ikilalamika kwenye vyombo vya habari kuwa ratiba hiyo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa March 30 itakuwa mkoani Shinyanga kucheza mchezo wa kombe la FA dhidi ya Stand United.

Simba inatarajiwa kucheza michezo mingine mitatu mwezi wa nne kama inavyoonekana hapa chini.

Mtibwa vs Simba Aprili 9
Lipuli FC vs Simba Aprili 20
Simba vs Yanga Aprili 29


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.