Morocco Ata Sababu Ya Kutojumuishwa Kwa Mkude Kwenye Kikosi Cha Timu Ya Taifa..
Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ , Hemed Morocco ameweka wazi sababu zilizopelekea kiungo wa kati wa klabi ya Simba Jonas Mkude kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichotangazwa hivi karibuni.
Morocco amesema moja ya sababu iliyopelekea Mkude kutotajwa ilikuwa ni kuwa patia nafasi na vijana wengine wenye vipaji kuonyesha walichonacho.
Kauli hiyo ya Morocco imekuja baada ya malalamiko makubwa kutoka kwa wapenzi wa kandanda nchini yaliyohusisha kukosekana kwa Mkude ambae kwa sasa ni mmoja wa kiungo bora zaidi hapa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Juzi Morocc alitaja wachezaji 22 wa timu ya taifa watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya kirafiki ya kimataifa inayotambuliwa na Shirikisho la Kandanda ulimwenguni FIFA dhidi Algeria DR Congo michezo itakayopigwa machi 22 na machi 27.
Ambapo katika nafasi ya viungo Morocco aliwataja, Hamisi Abdallah (AFC Leopards), Mudathir Yahaya (Singida United), Said Ndemla (Simba), Faisal Salum (JKU) na Abdulazizi Makame (Taifa Jang’ombe).
“Huo ndio uamuzi wa benchi la ufundi kwa michezo hii miwili ya kirafiki ya kimataifa."
“Tuna imani na wachezaji tuliowaita na ndio maana tumejaribu kuongeza sura mpya katika kikosi."
“Mkude amekuwa kwenye kikosi kwa muda sasa lakini tumejaribu kuwapatia vijana wenye vipaji nafasi ili waonyeshe vipaji ikiwa ni pamoja na kuongeza uzoefu katika michezo ua kimataifa." Alisema Morocco.
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.