Kimebakia Kibari Tu, Ulimwengu Kuanza Kuichezea Klabu Hii Ulaya. Meneja Kasongo Afunguka Ukweli Juu Ya Hili.


Baada ya kimya kirefu sasa rasmi kuwa Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na nyota wa Zamani TP Mazembe, Thomas Ulimwengu ametajwa kukamilisha uhamisho wa na klabu ya FK Tuzla ya Nchini Bosnia na Herzegovina Ulaya.

Ulimwengu ambaye amewahi kuichezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden amejiunga na klabu hiyo baada ya makubaliano yaliyofikiwa katika pande zote mbili baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Wakala wake Jamali Kasongo, aemesema kwa sasa wanangojea kibari cha kumruhusu kucheza kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Bosnia.


“Atacheza nchini Bosnia licha ya kuwa tulipokea ofa kutoka katika vilabu tofauti na endapo mambo yote yatakamilika tutawajuzeni." Alisema Kasongo.

FK Sloboda Tuzla ni klabu inayoshiriki ligi kuu ya Bosnia na Herzegovina na kwa sasa ipo katika nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi hiyo baada ya kujikusanyia pointi 21.

Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.