Raundi Ya 22 Ligi Kuu Tanza Bara Kuendelea Leo Mechi Mbili Zapanguliwa, Hii Hapa Ratiba Kamili.


Mzunguko wa 22 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaendelea leo kwa mechi tano (5) kupigwa katika viwanja tofauti.

Mechi hizo za mzunguko wa 22 zitakazochezwa leo  ni:-

AzamFC vs Mbao FC (Azam Complex,Chamazi)

Ruvu Shooting vs Mbeya City (Mabatini)

Singida United vs Ndanda (Namfua)

Majimaji vs Lipuli (Majimaji)

Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar (Sokoine)


Mechi mbili za mzunguko huo zilizokuwa zichezwe Machi 11, 2018 zimebadilishiwa, Simba SC waliokuwa wacheze ugenini dhidi ya Njombe Mji mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya wekundu hao wa Msimbazi kuomba kusogezwa mbele ili kupata muda wa maandalizi yao ya marudiano dhidi ya Al Masry Kombe la Shirikisho utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.

Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mechi yao dhidi ya Young Africans uliyochezwa juzi Machi 9, 2018.



Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.