Mbao Yakubali Kipigo Kutoka Kwa Wajelajela(Tanzania Prisons).


Mchezo wa kiporo wa Raundi ya 20 ya ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya wajelajela Tanzania Prisons na wabishi Mbao FC umemalizika baada ya hapo Jumamosi kushindwa kumalizika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika jijini la Mbeya.

Mchezo huo umemalizika kwa matokeo ya Tanzania Prisons kuichapa Mbao FC bao 1-0 bao ambalo lilipatikana kwa njia ya penati katika dakika ya 11 ya mchezo huo iliyofungwa na mshambuliaji kinda Mohamed Issa Rashid.

Kwa Mbao penati hiyo ni ishara mbaya kwa safu yao ya ulinzi kwani mpaka sasa wamefanya makosa yaliyozaa penati na kufungwa katika mechi dhidi ya Stand United, Ruvu Shooting, Singida United, Lipuli FC, Simba SC na sasa Tanzania Prisons huku penati dhidi ya Kagera Sugar ikiokolewa.

Matokeo hayo yanawafanya Mbao kusaliwa na alama 19 na kuendelea kuwa katika nafasi ya 12 wakati Tanzania Prisons wakifikisha alama 32 katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.