Stars Watolewa AWCON Kishujaa.
Timu ya soka ya Taifa kwa upande wa wanawake (Twiga Stars) imeshindwa kufuzu katika hatua ya pili ya michuano ya kuwania kufuzu kwenye fainali za mataifa Afrika licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na wenyeji timu ya soka ya Zambia (Shepolopolo) katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Nkoloma mjini Lusaka.
Shepolopolo ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tatu ya mchezo kupitia kwa Racheal Kundananji baada ya kazi nzuri ya Barba Banda kabla ya Twiga Stars kusawazisha katika dakika ya 68 kupitia kwa Donisia Daniel baada ya kuonganisha mpira wa Mwanahamis Omary 'Gaucho'.
Kwa matokeo hayo Tanzania wanatolewa kwa bao la ugenini baada ya kuruhusu sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na ikumbukwe hii ni kwa mara ya pili mfululizo Tanzania wakitolewa na Zambia katika michuano ya kufuzu kwenye fainali za mataifa Afrika.
Sasa Zambia watakutana na Zimbabwe katika hatua inayofuata baada ya wao kuwaondoa Namibia kwa jumla ya mabao 4-0 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa duru ya kwanza uliofanyika Jumapili hii.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.