TFF YAANZISHA TIMU ZA VIJANA:

TFF YAANZISHA TIMU ZA VIJANA: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanzisha ligi za vijana  kwa timu za  Ligi Kuu ya  Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja pili (SDL), kwa lengo la kukuza mchezo wa mpira wa miguu nchini, zikishirikisha vijana chini ya miaka 20, 17 pamoja na 15.
Ligi ya U20 itaanza Oktoba ikishirika timu za vijana (U-20) kwa vilabu vyote kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, huku Mashindano ya U17 yatakayoshirikisha timu 68 za vijana kutoka vilabu vya Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili yakitarajiwa kuanza Novemba, 2018.
Michuano ya U15 itashirikisha jumla ya timu 35 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ambayo inatarajiwa kuchezwa mwezi Disemba, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kamati ya mashindano wa TFF Salumu Madadi amesema  ligi hizo zitawapa vijana fursa ya kupata jukwaa la kuonesha vipaji vyao.