Mkusanyiko wa habari muhimu za soka Ulaya 04.08.2018



Arturo Vidal: Barcelona imefikia makubaliano na Bayern Munich kumsaini kiungo huyo wa kati.


Barcelona imeafikia makubaliano na Bayern Munich kumsaini kiungo wa kati wa Chile Arturo Vidal kwa mkataba wa miaka mitatu kwa dau lisilojulikana
Vidal, 31, atafanyiwa ukaguzi wa matibabu na miamba hiyo ya Uhispania katika siku chache zijazo.
Alijiunga na Bayern kutoka Juventus mwaka 2015 na kushinda taji la Bundesliga katika misimu yake yote mitatu nchini Ujerumani
"Barcelona itatangaza kuhusu kuwasili kwa mchezaji huyo na ajenda ya kumzindua , Barca ilisema katika taarifa.
Fifa yamruhusu Saido Berahino kuichezea Burundi
Neymar aingia kama nguvu mpya huku PSG ikiishinda Monaco katika kombe la Supercup


Neymar aliingia kama nguvu mpya kwa PSG huku timu yake ikiilima Monaco 4-0 katika kombe la Ufaransa la Super Cup.
Mechi hiyo nchini China ilikuwa ya kwanza kwa mshambuliaji huyo wa Brazil tangiu kombe la dunia na ya kwanza tangu Februari , wakati alipopata jeraha la mguu
Neymar aliingia baada ya dakika 75 katika mechi katika ya viongozi wa ligi na mabingwa watetezi wa kombe la Supercup.
Angel Di Maria alifunga magoli mawili huku Christopher Nkunku na Timothy Weah wakifunga magoli mengine ya Penati

Samuel Eto'o aondoka katika klabu ya Uturuki ya Konyaspor kwa makubaliano


Nahodha wa zamani wa Cameroon Samuel Eto'o ameondoka katika klabu ya Konyaspor kwa makubaliano huku ikiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake.

Klabu hiyo ya Uturuki inasema kuwa kandarasi ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Everton ,37 imefutiliwa mbali kutokana na makubliano ya awali.

Eto'o alijiunga na Konyaspor kutoka kwa wapinzani wao Antalyaspor mnamo mwezi Januari, akifunga magoli sita katika mechi 14 ili kuisaidia klabu hiyo kuimarisha uongozi wake.

Klabu hiyo imemshukuru kwa huduma zake.

Mchezaji wa Everton Kevin Mirallas kuhamia Fiorentina kwa mkopo


Winga wa Everton Kevin Mirallas anatarajiwa kujiunga na Fiorentina kwa uhamisho wa mkopo wa muda mrefu, akitarajia kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.

Hatua hiyo imetangazwa siku moja baada ya Everton kutangaza idadi ya wachezaji wake na kumpatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 tisheti yenye nambari nane.

Mirallas alihudumu kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo baada ya kuelekea katika klabu hiyo ya Ugiriki mnamo mwezi Janurai.

Hatahivyo alishindwa kushirikishwa katika kikosi cha Ubelgiji cha kombe la dunia 2018 na sasa anatarajiwa kuondoka kuelekea katika klabu hiyo ya Itali.

Kadi nyekundu na ya njano kwa mameneja wa soka watovu wa nidhamu

Cameroon yamuajiri Seedorf na Kluivert baada ya makubaliano na Eriksson kwenda mrama.

Clarence Seedorf ameteuliwa kuwa mkufunzi mpya wa Cameroon baada ya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Uingereza kufeli.
Kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid, AC Milan na Uholanzi Seedorf atasaidiwa na mchezaji mwenza wa zamani Patrick Kluivert.

Kiwango cha kanadarasi ya Seedorf na mabingwa hao mara tano wa Afrika kitatangazwa baadaye mwezi huu.
Seedorf mwenye umri wa miaka 42, ameifunza AC Milan, klabu ya China ya Shenzhen na Deportivo Lacuruna.
United yaiangamiza Real Madrid, Barcelona hoi kwa Roma
Salomon Rondon: Newcastle inakaribia kumsaini mshambuliaji huyo wa West Brom.

Newcastle inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon kutoka West Brom.
Klabu hizo mbili zimekuwa zikifanya mazungumzo ya kuweka mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambao unatarajiwa kukamilishwa wikendi.
Randon hakushirikishwa katika kikosi cha West Brom kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Bolton Jumamosi

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.