Kocha Gor Mahia Awapa Neno Simba Kuelea Mchezo Dhidi Ya Al-masry



Kocha wa zamani wa Simba SC ambaye kwa sasa ana kinoa kikosi cha  Gor Mahia FC ya Kenya, Dylan Kerr, ametoa ushauri wake kwa klabu ya Simba kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry SC.

Simba ipo safarini hivi sasa kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii.

Kerr amesema inabidi benchi la ufundi chini ya Kocha Pierre Lechantre, lisitumie mfumo wa kujilinda na badala yake wafunguke ili kupata mabao ya mapema.

Aidha Kerr ameeleza, Simba wanapaswa kutoruhusu bao la mapema kwani itawapa ugumu kusonga mbele kulingana na desturi ya soka la Waarabu namna lilivyo.

"Wanapaswa kutoruhusu bao la mapema kwasababu mchezo utakuwa mgumu kwao, pia hawapaswi kujilinda, wafunguke ili wapate matokeo ya mapema" amesema Kerr.

Hajaishia hapo, Kerr amewaomba pia wachezaji wa Simba watambue thamani wa timu yao, akiwataka wapambane kwa nguvu zote, wajue kuwa kuna mashabiki wao wanatagemea matokeo mazuri.

"Simba wanapaswa kupambana, wajue kuwa kuna mashabiki wanawatazama, wajitume kwa nguvu zao zote" alisema.
Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.