KIGOGO TFF KUFUNGIWA MAISHA KWA KOSA HILI...


Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu TFF, Michael Wambura, amekumbwa na kashfa ya tuhuma za kujilipa fedha isivyo halali. Na jana amejadiliwa na kamati ya Maadali na habari za uhakika kutoka kwenye kikao hicho Michael Richard Wambura atafungiwa kujihusisha na Soka maisha.

-Wambura amekutwa na hatia kwa Makosa yote matatu kosa la kwanza ni Kupokea Fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kosa la pili Kughushi barua ya kuelekeza malipo ya kampuni ya JECK SYSTEM LIMITED, huku la tatu ni kushusha hadhi ya shirikisho kwa alichokifanya kwenye makosa namba 1,2.

-Wambura ambaye hayupo nchini aliwakilishwa na Wakili Emmanuel Mganyizi ambaye alikana tuhuma zote juu ya mteja wake. Ila baadae kamati ya maadili ilijiridhisha Michael Wambura kutenda makosa hayo na sasa atafungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya Mpira.

-Wambura anadaiwa kujilipa Dola za Marekani 45,000 (Dola moja inauzwa Sh 2,240), kwa nyakati tofauti ikiwa ni fedha ambazo Kampuni ya Jecks Systerms Limited iliikopesha iliyokuwa FAT, sasa TFF mwaka 2002 akiwa Katibu Mkuu.

-Kwa mjibu wa makubaliano ya mkopo kati ya mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Enock Maganga (sasa marehemu) na Wambura kama Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, yalisainiwa Novemba 29, 2002 ikiwa ni mkopo wa dola za Marekani 30,000 kwa makubaliano ya kurudisha dola 45,000.

-Mjane wa Maganga, Irene Maganga ambaye yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya mumewe aliyefariki kwa tatizo la figo nchini India, ndio aliyeibua deni hilo kwa vile alikuwa akilifahamu, na ndipo alipobaini fedha zao zimelipwa na zimeliwa na Wambura.

-Kwa mujibu wa makubaliano ya mkopo huo, ambapo nyaraka zinadai ulikuwa ni kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, FAT ilitakiwa kurejesha na riba ya dola za Marekani 15,000.

-Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya TFF, zilibainisha kuwa fedha hizo zilishalipwa zote kwa awamu kati ya mwaka 2002 na mwaka 2015, na fedha iliyotoka ni zaidi ya kiasi kilichokuwa kikidaiwa na kampuni hiyo.

-Fedha zilikuwa zinalipwa kwa awamu kwa Wambura ambaye baadaye alijitambulisha kama mmoja wa wakurugenzi wa Jecks na mpaka deni hilo linakwisha, zilikuwa zimeshalipwa sh milioni 84,

-Malipo ya awali yalifanyika wakati yeye (Wambura) akiwa kiongozi, na kisha baada ya kuingia uongozi wa Leodegar Tenga, hakuna malipo yoyote aliyodai mpaka Tenga alipoondoka madarakani mwaka 2013, ndipo alipokuja kudai tena akidai aliikopesha TFF fedha hivyo anataka alipwe.

-Kwa mujibu wa nyaraka za malipo zilizosainiwa na Wambura Julai 30, 2004, Makamu huyo wa Rais wa TFF alilipwa Sh milioni 16.5 kwa vocha namba 5324 ambazo malipo yalifanyika kwa fedha taslimu.

-Aidha, kwa mujibu wa nyaraka hizo, malipo mengine yalifanyika Agosti 15, 2014, Wambura kupitia kampuni hiyo alilipwa Sh 10,050,200 kwa vocha namba 009647 na hundi namba 02059, Oktoba 2, mwaka huohuo alilipwa Sh milioni 5 kwa vocha namba 00790 na namba ya hundi ni 00848, Oktoba 21 Sh milioni 10 kwa vocha namba 00810 na hundi namba 00319

-Kisha malipo mengine yakafanyika mwaka 2015 ambako Machi 16, alilipwa Sh 10,001,930 kwa vocha namba 0011071 na hundi namba 002271, Juni 16 alilipwa Sh milioni 10 kwa vocha namba 001226 na hundi namba 0026, Julai 25 Sh 5,095,424 kwa vocha namba 001187 na hundi namba 002408.

-Malipo mengine ni Agosti 19 alilipwa Sh milioni 2 kwa vocha namba 001641 na hundi namba 000583, Septemba 14 Sh milioni 3 kwa vocha namba 003601 na hundi namba 00445 na malipo ya mwisho yalifanyika Septemba 30, 2015 ambako zililipwa Sh 12, 352,500 kwa vocha namba 003650 na hundi namba 000497.

-Baada ya tuhuma Hizo Sekretarieti ya TFF ilimpeleka Michael Richard Wambura Makamu wa Rais wa TFF kwenye kamati ya Ukaguzi wa fedha ambayo inaongozwa na Athumani Nyamulani na iliona kuna ukweli kuhusu tuhuma hizo za Makamu Rais wa TFF ndipo shauri hilo lilipelekwa kamati ya Maadili ya TFF kamati ambayo Nyamulani ni Mjumbe.

-Muwakilishi wa Wambura, Wakili Emma Mga amedai kuna hila zinafanywa baada ya viongozi wa TFF ambao hawamtaki Michael Richard Wambura ndio maana wameamua iwe hivyo. Wakili huyo amedai hakukuwa na Ulazima wa kumvizia Wambura yuko nje ya nchi wakae kikao.

-Habari za kuaminika Richard Wambura amesitisha shughuli zake na anatarajia kuwepo Tanzania kuanzia majira ya saa 4 asubuhi leo. Ila kamati imemaliza tayari kumjadili Wambura kinachosubiliwa ni kutolewa kwa taarifa tu.

@yossima jr

Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.