AKILIMALI AIBUKA NA HILI YANGA



-Katibu wa Baraza la wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amewakumbusha viongozi wa Yanga kuhusu uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti aliyejiuzulu.

-Akiongea leo amedai uongozi wa Yanga unaendelea kuvunja katiba na kanuni za klabu hiyo kwa kushindwa kutangaza mchakato wa kuanza kujaza nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo.

"Nawakumbusha viongozi wangu kujaza nafasi ya mwenyekiti ambayo Mbwana Yusuph Manji alijiuzulu mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita nafasi hiyo haijajazwa na katiba yetu inasema miezi sita tu mtu akijiuzulu lazima ijazwe"

"Kaimu Mwenyekiti wa klabu Clement Sanga yupo kimya, Katibu wa klabu naye yupo kimya, kamati ya utendaji iko kimya hata kamati ya uchaguzi  ipo kimya tunaendelea kuvunja matakwa ya katiba yetu sasa ni muda wa kujaza nafasi hiyo"
   Alisema Mzee Akilimali

-May 2017, Yusuph Manji alijiuzulu nafasi ya mwenyekiti na nafasi zote za uongozi ndani ya klabu ya Yanga. Kuna kipindi uongozi wa Yanga ulitangaza Yusuph Manji amerejea ndani ya kikosi hicho.

@yossima Sitta Jr.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.