Tshishimbi Atoa Onyo Kali Yanga...


Kiungo wa klabu ya Yanga Papy Kabamba Tshishimbi atoa onyo kali kwa wenzake kuwa makini kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa klabu bingwa afAfri dhidi St Louis utakaopigwa Jumatano.
Katika Mchezo wa awali Yanga iliibuka kidedea kwa goli 1-0 dhidi ya St. Louis kwa goli liliopachikwa  kimiani na Emmanuel Martine.
"Tuanahitajika kuwa makini na kuwaheshimu wapinzani wetu kwa sababu wapo katika uwanja wao wa nyumbani , lakini Yanga ni timu kubwa tunahitajika kuthibitisha hilo kwa kupata ushindi  na kufuzu katika hatua nyingine" Alisema Tshishimbi.
Tshishimbi ameangeza kwa kusema kuwa mchezaji yeyote atakaye anza basi atahakikisha anapambana  kuhakikisha wanajangwani wanaibuka na ushindi.

Yanga wameondoka jana Asubuhi kuelekea Shelisheli bila starika wake Obrey Chirwa ambae ameachwa kutokana na majereha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Majimaji fc.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.