Dr Bavu Awataja Wachezaji Yanga Watakaoikosa Majimaji Fc Leo..


Klabu ya Yang sc imekamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya MajiMaj Fc mchezo unaotarajiwa kupigwa leo kwenye uwanja wa Taifa.

Daktari wa timu hiyo Dr Edward Bavu amethibitisha kuwa nyota wanne pekee ndiyo hawatakuwa sehemu ya mchezo huo wa leo
Dr  Bavu amesema kuwa, Amissi Tambwe,Yohana Mkomola, Donald Ngoma na Abdallah Shaibu ni wachezaji ambao bado wako kwenye majeraha na watasalia nje kupisha dakika 90 za mchezo huo.


Ni vigumu kuwatumia,bado wanauguza majeraha, kama klabu tunafanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa wanarejea uwanjani kuanza kucheza, si jambo jema mchezaji kukaa nje muda mrefu, kuna wakati majeraha huamua hii ni kwa sababu mpira wa miguu una matukio mengi uwanjani, ni wazi tutawakosa mchezo Majimaji.

Kuhusu kiungo Thabani Kamusoko,Dr Bavu alisema kuwa mchezaji huyo ameshapona majeraha yake na tayari amekwisha anza mazoezi mepesi kwa ajili ya kuweka sawa utimamu wa mwili.


Kucheza mechi ni jambo ambalo linahitaji utimamu wa mwili asilimia mia moja,jambo jema ni kuwa mchezaji tayari kashaanza mazoezi, hii inamaana kuwa wakati wowote anaweza kurejea uwanjani.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.