Amka Na Taarifa Hizi Kutoka Azam FC Leo 19.02.2018


Baada ya mapumziko ya jana Jumapil, leo kikos cha Klabu ya Azam FC, kitaanza rasmi maandalizi kuelekea mchezo ujao wa Kombe la SHirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya KMC utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi ijayo (Februari 24) saa 1.00 usiku.

Azam FC imefika raundi hiyo ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya kuichapa Shupavu mabao 5-0 huku KMC ambayo imeshapanda Ligi Kuu kuelekea msimu ujao, iliichapa Toto Africans 7-0.

Katika hatua nyingine klabu ya Azam itaikosa huduma ya kiungo wake na nahodha wa klabu hiyo, Himid Mao ambae yuko nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu ya majeraha aliyopata.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka bondeni zinaeleza kuwa Himid Mao amegundulika na uvimbe katika goti lake na atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu akipata matibabu.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.